Dosari za Kifonolojia Zinazojitokeza kwa Wangoni Wanapojifunza Kiswahili

Authors

  • Arnold Gawasike Msigwa Author
  • Edward Shanel Nyoni Author

Keywords:

Dosari, kifonolojiia, Kiswahili, Wangoni

Abstract

Utafiti huu ulichunguza dosari za kifonolojia zinazojitokeza kwa
jamii ya Wangoni wanapojifunza Kiswahili. Tatizo la utafiti
lilichochewa na watafiti wengi kutafiti dosari kwa Wabantu
wanapojifunza lugha ya pili yenye mfumo tofauti na lugha yao ya
kwanza. Utafiti uliongozwa na Nadharia ya Uchanganuzi Dosari ya
Corder (1967)inayoeleza kwamba dosari katika ujifunzaji wa lugha
ya pili hazitokani tu na mifumo tofauti kati ya lugha ya kwanza na
lugha ya pili, bali kuna masuala anuwai mengine yanayomzunguka
mjifunzaji na kuchangia kuibuka kwa dosari. Utafiti ulikusanya
data katika wilaya ya Songea vijijini katika shule za sekondari
Nalima na Liganga. Utafiti ulihusisha jumla ya watoataarifa 24
ambao ni wanafunzi wanaosoma kidato cha tatu pamoja na walimu
wanaofundisha Kiswahili katika shule hizo. Mbinu zilizotumika
kukusanya data ni majadiliano ya kundi na hojaji. Uchambuzi wa
data za utafiti huu umetumia mbinu ya maelezo ambapo dosari zote
zilizobainika ziliwekwa katika makundi maalum na kutolewa
maelezo kikamilifu. Matokeo yanaonesha kwamba zipo dosari za
kifonolojia zinazojitokeza kwa Wangoni wanapojifunza Kiswahili,
hususani upachikaji wa sauti, mfano neno, afurika, sauti /u/
inapachikwa ubadilishaji wa sauti, mfano miladi badala ya
‘’miradi’’ na udondoshaji, mfano neno akuna badala ya ‘hakuna’.
Ili kuwafanya wajifunzaji hawa wajifunze Kiswahili kwa usahihi,
ilipendekezwa kuwa, kuwepo na mchanganyiko wa wanafunzi
kutoka ndani na nje ya mkoa katika shule za kata, kuwepo kwa
midahalo, makongamano na majarida ya Kiswahili ya kutosha, pia
yafanyike mazoezi shirikishi kwa shule zaidi ya moja

Cover Image

Downloads

Published

2025-12-26

Most read articles by the same author(s)

<< < 1 2