Uchanganuzi Amilifu-Zalishi Wa Miundo Ya Kimofolojia

Authors

  • Salim Sawe Author
  • Mosol Kandagor Author

Keywords:

Nyuklia, Satalaiti, Uamilifu, Uzalishi, Kategoria za kimofolojia

Abstract

Makala hii ni uchanguzi amilifu-zalishi wa miundo ya
kategoria za kimofolojia. Inachunguza utata unaotokea katika
ufafanuzi wa dhana ya neno na aina za maneno katika
Kiswahili. Utata huu unatokana na mitazamo tofauti ya
wanasarufi kuhusu aina za maneno kama kategoria za
kimofolojia, ambapo wengine wanabainisha aina saba, na
wengine nane. Data inayochanganuliwa katika makala haya
imekusanya mazungumzo ya Kiswahili sanifu kwa kutumia
usampulishaji wakilishi wa kimakusudi. Nadharia Amilifu
Zalishi (NAZ) inasisitiza uamilifu wa viambajengo katika
kuunda miundo ya kisarufi, ikihusisha fonolojia, mofolojia,
na sintaksia. Aidha, makala inaeleza kwamba neno linaweza
kufasiliwa kwa njia mbalimbali, ikiwa ni pamoja na njia ya
kiothografia, kifonolojia, kimofolojia, kisemantiki, na
kisintaksia. Matokeo yanaonesha kuwa ubainishaji wa aina
za maneno unapaswa kuzingatia uhusiano kati ya kategoria
mbalimbali, na kwamba neno linaweza kuwa na maana
tofauti kulingana na muktadha wa matumizi. Kwa hivyo,
makala inatoa mchango mkubwa katika kitengo cha Isimu
Fafanuzi na Isimu Nadharia.

Cover Image

Downloads

Published

2025-12-26

Most read articles by the same author(s)

<< < 1 2