Uashiriaji Wa Kijinsia Kama Suala Mahususi La Kitamaduni: Mchango Wa Uashiriaji Wa Kijinsia Katika Mwachano Wa Maana Kwenye Tafsiri Za Nyimbo

Authors

  • Edward Mariga Author

Keywords:

Tafsiri, Jinsia ya Kisemantiki, Jinsia ya Kisarufi, Nadharia ya Wingimifumo na Masuala Mahususi ya Kitamaduni

Abstract

Makala haya yanachunguza jinsia kama suala mahususi la kitamaduni katika tafsiri zinazofanywa kutoka Kiingereza kwenda Kiswahili na kwa msingi huo kubaini nafasi ya uashiriaji wa kijinsia katika mwachano wa maana katika tafsiri za aiana hiyo. Suala mahususi la kitamaduni likimaanisha suala linalopatikana katika lugha moja na kukosekana katika lugha ya pili katika tafsiri. Utafiti ulichochewa na mwelekeo wa tafiti za awali kuwa tofauti za maana katika tafsiri ni matokeo ya upungufu katika tafsiri. Utafiti huu ulichukua mwelekeo kuwa si tofauti zote za maana katika tafsiri ni ishara ya uchapwa katika tafsiri husika. Matini zilizochunguzwa katika utafiti huu ni pamoja na ‘Nyimbo za Kristo’ kama matini lengwa na matini chasili ‘The Seventh Day Adventist Hymnal’ ambapo data zilikusanywa kwa njia ya uchanganuzi matini. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya wingimifimo ya Gideon Touri (1980). Utafiti huu ulihusu eneo la fasihi tafsiri ambapo usampulishaji dhamirifu ulitumika. Kati ya nyimbo 220 katika matini lengwa zilizochunguzwa, 116 zinazodhihirisha masuala ya kijinsia zilifanyiwa uchanganuzi linganuzi ili kubaini masuala ya kitafsiri yaliyoibuka kuhusu jinsia. Matokeao ya utafiti yalionyesha kuwa jinsia ni suala mahususi katika tafsiri zinazofanywa kutoka Kiingereza kwenda Kiswahili na hivyo kuchangia mwachano wa maana. Aidha, utafiti ulionyesha kuwa tofauti za maana kati ya matini mbili husika zilizohusishwa na masuala ya kijinsia, hazikutokana na upungufu wa kitafsiri bali tofauti katika uashiriaji wa kijinsia kati ya lugha mbili husika. 

Cover Image

Downloads

Published

2026-04-24

Most read articles by the same author(s)

<< < 1 2