Falsafa ya Ubuntu katika Riwaya za Kisasa za Kiswahili

Authors

  • Bakita Malindi Author
  • Dkt. Mohamed Maguo Author
  • Dkt. Anna Kyamba Chuo Kikuu Huria cha Tanzania- Dar es Salaam, Tanzania Author

Keywords:

Falsafa ya Ubuntu, riwaya za kisasa za Kiswahili

Abstract

Makala hii inahusu falsafa ya Ubuntu katika riwaya za kisasa za Kiswahili. Makala hii imelenga kubainisha vipengele mbalimbali vya falsafa ya Ubuntu vinavyojitokeza katika riwaya za kisasa za Kiswahili. Riwaya teule zilizotumika wakati wa ukusanyaji wa data na uchanganuzi wake ni riwaya ya Babu Alipofufuka (2001) na Makuadi wa Soko Huria (2002). Riwaya hizi zimeteuliwa kwa kuwa ziliandikwa kati ya mwaka 2001 hadi 2005 kipindi ambacho utandawazi ulizungumziwa kwa kiasi kikubwa na wanazuoni wengi katika fasihi ya Kiswahili. Vilevile riwaya hizo teule zinaakisi vizuri hali halisi ya falsafa ya Ubuntu katika nchi za Kiafrika katika zama hizi za utandawazi. Data za makala hii zilipatikana kwa kutumia mbinu ya usomaji makini wa matini. Aidha, data zilichambuliwa kwa kutumia mkabala wa kitaamuli, ambapo maelezo yalitumika kuwasilisha uchambuzi wa data. Nadharia ya Ontolojia ya Kibantu imetumika katika uchambuzi na uwasilishaji wa data. Matokeo ya utafiti wa makala hii yamebainisha vipengele mbalimbali vya falsafa ya Ubuntu vilivyojitokeza katika riwaya teule za kisasa za Kiswahili. Halikadhalika, yameonesha kuwa riwaya za kisasa za Kiswahili zimezungumzia pia falsafa ya Ubuntu inayoendana na utandawazi katika ulimwengu huu wa sasa, ingawa kuna tafiti zinazosema falsafa ya Ubuntu imepunguka ama kuporomoka kabisa katika zama hizi za usasa (Jean, 2002; Oni, 2005)

Author Biographies

  • Bakita Malindi

    Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere- Dar es Salaam, Tanzania

  • Dkt. Mohamed Maguo

    Chuo Kikuu Huria cha Tanzania- Dar es Salaam, Tanzania

  • Dkt. Anna Kyamba, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania- Dar es Salaam, Tanzania

    Chuo Kikuu Huria cha Tanzania- Dar es Salaam, Tanzania

Downloads

Published

2026-11-03

Issue

Section

Articles

Most read articles by the same author(s)

<< < 1 2 3 > >>