Uteuzi na Uwiano wa Maneno Katika Methali: Mfano wa Methali za KiswahiliZinazorejelea Uhusiano wa Kiudugu
Keywords:
akisi, methali, muktadha, uamilifu, uteuzi na uwianoAbstract
Utafiti huu wa kiisimu unalenga kubainisha na kufafanua
jinsi uteuzi wa maneno unavyowiana na kushikamana
katika methali za Kiswahili. Aidha, utafiti huu
unachunguza muktadha na uamilifu wa uteuzi wa maneno
hayo katika kuakisi matumizi ya methali za Kiswahili
zinazorejelea uhusiano wa kiudugu. Utafiti huu ni matokeo
ya data za uwandani za usaili na ushuhudiaji. Mbinu zote
hizo kwa pamoja zimemsaidia mtafiti kupata data
toshelevu za kujibu lengo la makala hii. Makala hii,
imeongozwa na Nadharia ya Mahusiano iliyoasisiwa na
Sperber na Wilson (1995). Katika nadharia hiyo mbali na
mambo mengine, inazungumzia namna maneno
yanavyohusiana katika tungo hadi kupata maana
iliyokusudiwa na msemaji kwa msikilizaji. Vilevile, katika
makala hii data zimewasilishwa kwa kutumia mkabala wa
kitaamuli. Kwa ujumla, matokeo ya uchunguzi yameweka
bayana uteuzi na uhusiano wa maneno kwa lengo la
kuakisi uamilifu wa methali hizo za Kiswahili kulingana
na muktadha husika. Hivyo, tunapendekeza watafiti
wengine wafanye ulinganishi wa methali za Kiswahili na
methali za lugha nyingine za Kiafrika. Ulinganishi ambao
utaangazia suala la uteuzi na uwiano wa maneno pamoja
na uamilifu uliomo katika methali mbalimbali za Kiswahili
na lugha za Kiafrika.
Downloads
Published
Issue
Section
License
Copyright (c) 2026 Africa Journal of Language Studies

This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License.