Uamilifu wa Sifa katika Mfumo wa Fonimu Konsonanti za Kiswahili

Authors

  • David Majariwa Department of Kiswahili, Kabale University Author

Keywords:

Uamilifu, Sifa, Mfumo wa fonimu

Abstract

Makala haya yanachunguza uamilifu wa sifa bainifu katika mfumo wa fonimu konsonanti za Kiswahili. Uhakiki wa mfumo wa fonimu konsonanti za Kiswahili ili kubainisha uamilifu wa sifa katika orodha ya fonimu za Kiswahili umeelezwa kwa kuzingatia michakato ya upokeaji wa maneno yenye asili ya Kiarabu mkiwamo vitamkwa [θ], [ð], [χ] na [ɣ]. Uchunguzi huu ulijikita katika misingi ya uhakiki wa orodha ya vitamkwa ambayo ni Udhibiti wa sifa, Iktisadi ya sifa, Uziada, Utabakishi wa sifa na Uzidishaji wa sifa iliyotolewa na Clements (2003). Data zilikusanywa kutoka Kamusi ya Kiswahili Sanifu, Toleo la 3 na Bosha (1993). Data zilikusanywa kwa njia ya uchanganuzi matini. Matokeo ya uchunguzi huu yanaonesha kuwa kuna misingi inayodhibiti sifa bainifu za fonimu konsonati za Kiswahili. Kwa ujumla, misingi hii inashirikiana kuukilia kaida za mfumo wa fonimu za Kiswahili kama uelekeo wa msambao wa fonimu na nafasi za kutamkia. Aidha, matokeo yanaonesha kuwa fonimu za Kiswahili zinadhihirisha ruwaza wiani katika mfumo huo. Makala haya yanatoa mchango kwa kubainisha iktisadi kwenye uamilifu wa sifa katika mfumo wa fonimu konsonanti za Kiswahili.

Downloads

Published

2024-12-06

Issue

Section

Articles

Most read articles by the same author(s)