Kanuni za Mfuatano wa Mofu za Utendeka na Utendana katika Kitenzi cha Kihehe

Authors

  • Asia Mashaka Akaro Author

Keywords:

Mfuatano wa Mofu, Utendeka, Utendana

Abstract

Makala haya yanahusu Kanuni za Mfuatano wa Mofu za Utendeka na Utendana zinazojidhihirisha katika vitenzi vya lugha ya Kihehe. Mfuatano wa mofu ikiwa ni namna mofu hizo zinavyojipanga katika kujenga vitenzi kubalifu vya lugha ya Kihehe. Tatizo lililomsukuma mtafiti kufanya utafiti huu ni kukosekana kwa utangamano miongoni mwa wataalamu kama vile: Mpalanzi (2010) kuhusu ruwaza za mfuatano wa utendeka na utendana katika mofu nyambulishi katika lugha ya Kihehe. Data za utafiti zilikusanywa katika wilaya ya Mufindi kwenye kata za Lungemba na Isalavanu katika vijiji vya Lungemba, Munyigumba na Maduma. Miongoni mwa sababu za kuteua eneo hili ni kuwa; kijiografia maeneo haya yako pembezoni mwa miji mikubwa, hivyo, mwingiliano na jamii zingine ni mdogo na hivyo yameihifadhi Kihehe asilia. Pia, haya ndiyo maeneo yanayosadikiwa kuwa ni asili ya lugha ya Kihehe. Zaidi ya hayo, lahaja ya maeneo haya ndiyo lahaja ya mtafiti, hivyo, ilirahisisha mawasiliano wakati wa ukusanyaji data na watoa taarifa. Sampuli ya utafiti ilikuwa ni watu sabini na wawili (72). Utafiti huu uliongozwa na Kanuni Akisi ya Baker (1985) inayosema kuwa mpangilio wa mofu kimofolojia ni lazima ushabihiane na mfuatano wa mofu kisintaksia kutegemea lugha husika. Hii ina maana kuwa iwapo kitenzi fulani kitapitia michakato miwili ya unyambulishaji kama vile, unyambulishaji tendea na tendana, mofu tendea lazima itokee karibu na mofu mzizi kuliko mofimu tendana. Njia za ukusanyaji wa data zilizotumika ni mahojiano na hojaji. Matokeo ya utafiti yanaonesha unyambulishaji tendeka unawakilishwa na mofu //-isik-// katika vitenzi vya silabi moja na mofu //-ik-// kwa vitenzi vyenye silabi zaidi ya moja. Wakati maumbo ya utendana ni mofu //-kwi-// na mofu //-an-//; mofu /-kwi-// inatokea kabla ya mzizi wa kitenzi wakati mofu //-an-// huja baada ya mzizi wa kitenzi. Aidha, kanuni zinazoongoza utokeaji wa maumbo hayo zimeelezwa katika makala haya.

Downloads

Published

2024-12-06

Issue

Section

Articles

Most read articles by the same author(s)